|
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akionyesha mfano wa hati ya
safari ya kuelekea Mwanza kupitia Shirika la ndege la Tanzania (ATCL), kushoto
kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa.
|
|
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiongea na waandishi wa
habari kabla ya kufanya ziara ya kikazimkoani Mwanza kupitia Shirika la ndege
la Tanzania (ATCL), leo jijini Dar es salaam.
|
|
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akipokea maoni kutoka kwa wasafiri
wanaotumia usafiri wa anga katika uwanja wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere
(JNIA) wakati alipokagua utoaji wa huduma uwanjani hapo.
|
|
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akipokea maoni kutoka kwa wasafiri
wanaotumia usafiri waa anga katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere wakati
alipotembelea kukagua huduma zitolewazo uwanjani hapo.
|
|
Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la ndege Tanzania (ATCL) Eng. Ladislaus Matindi akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa wakati alipotembelea Uwanja wa Kimataifa wa
Mwl. Julius Nyerere (JNIA) kukagua huduma zitolewazo uwanjani hapo.
|
|
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa wahudumu wa
ndege katika Chuo cha Shirika la ndege Tanzania (ATCL) alipotembelea kuona
maendeleo ya chuo hicho.
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Bi Samia Suluhu amewasihi viongozi wa serikali na wananchi
kutumia ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATC), ili kudumisha uzalendo na kuchangia
pato la shirika hilo kwa lengo la kuhimili ushindani na kukuza uchumi wa nchi.
Ametoa rai hiyo jijini
Dar es salaam alipopewa hati ya kusafiria kupitia ndege za shirika hilo wakati akisafiri
na ujumbe wake kuelekea mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi.
“Napenda kutoa wito kwa
viongozi wa Serikali na wananchi kwa ujumla kutumia ndege zetu ili shirika letu
lifanye kazi vizuri zaidi, kufanya hivi kutaongeza pato na kukuza uchumi wa nchi”,
amesema Makamu wa Rais.
Ametanabaisha kuwa kwa
kutumia ndege za Shirika la ATC kwa safari za ndani Serikali itaokoa fedha nyingi
zinazotumika kwa kukodi ndege za mashirika binafsi.
“Mimi na ujumbe tumeamua
kusafiri na ndege za shirika la ndege Tanzania kutokana na kubana matumizi, gharama
tuliyotumia kwa safari hii ni shilingi Milioni saba na laki sita ambapo tungekodi
ndege binafsi tungetumia milioni arobaini”, amefafanua Makamu wa Rais.
Kwa upande wake Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amempongeza Makamu huyo
kwa kitendo cha uzalendo alichokionyesha na kutaka viongozi wengine wa Serikali
na wananchi kwa ujumla kuiga mfano huo ilikuliinua shirika hilo na kuongeza uchumi.
“Nampongeza Makamu wa Rais
kwa kuamua kutumia ndege za Shirika hili kwa safari za ndani, kitendo hiki kimeonesha
nia ya dhati ya serikali ya kulifufua shirika hili, naomba wananchi nao waendelee
kutumia ndege za shirika hili katika safari zao za ndani kama alivyofanya Makamu
wa Rais”, amesema Waziri Mbarawa.
Naye Mkurugenzi Mtendaji
wa Shirika hilo Mhandisi Ladislaus Matindi ameahidi kuboresha huduma katika shirika
hilo ikiwemo mifumo ya kukatisha tiketi ili kurahisisha utoaji wa huduma na kuvutia
wateja wengi kwa lengo la kurudisha hadhi ya shirika.
“Tumeshaanza mchakato wa
kuweka mfumo mpya wa kukatisha tiketi ikiwemo kwa njia ya kielektroniki kupitia
tovuti ya shirika hili ambapo mteja hatalazimika kufika kwenye ofisi zetu”,
amesema Mhandisi Matindi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni