Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kulia), akizungumza na Balozi wa
Misri nchini, Yasser Elshawaf kuhusu masuala mbalimbali ya Sekta ya Miundombinu
ofisini kwake jijini Dar es salaam.
Balozi wa Misri
nchini, Yasser Elshawaf (kushoto), akifurahi jambo na Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa,
alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es salaam kuzungumzia masuala mbalimbali
kuhusu Sekta ya Miundombinu nchini.
Balozi wa Canada
nchini, Ian Myles (katikati), akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, alipomtembelea ofisini kwake kuzungumzia
masuala mbalimbali kuhusu Sekta ya Miundombinu nchini.
Mtaalam wa kurusha roboti
ya ndege (Drone) kutoka Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) (Watatu kushoto),
Bw. Fredrick Mbuya akitoa ufafanuzi wa namna
zoezi la kupiga picha katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)
lilivyotekelezwa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame
Mbarawa (wa kwanza Kulia). Hatua hiyo itaiwezesha Serikali kumaliza mgogoro wa
ardhi kati ya KIA na wananchi katika eneo hilo.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, akikagua roboti ya ndege (Drone)
iliyotumika katika zoezi la kupiga picha katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Kilimanjaro (KIA). Kushoto ni Katibu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania
(TCAA), Vallery Chamulungu.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, akifatilia kwa makini maelezo ya
Mtaalam wa kurusha roboti ya ndege (Drone) kutoka Tume ya Sayansi na Teknolojia
(COSTECH), Fredrick Mbuya, wakati akipokea taarifa ya awali kuhusu zoezi la
kupiga picha katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Mkurugenzi Mkuu wa Tume
ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Hassan Mshinda akimuonesha Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ramani ya eneo la uwanja
wa ndege wa KIA, baada ya zoezi la kupiga picha kukamilika.