Jumatano, 26 Oktoba 2016

PROF. MBARAWA AZINDUA BODI YA WAKURUGENZI YA SHIRIKA LA POSTA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akifafanua jambo kwa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta katika uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Prof. Faustin Kamuzora akisoma taarifa ya utekelezaji wa Shirika la Posta kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa katika uzinduzi wa  Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika hilo uliofanyika jijini Dar es salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Dkt. Haruni Kondo akisoma taarifa ya uendeshaji wa Shirika hilo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa katika uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam.

Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa katika uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akikata utepe kwenye begi lilobeba vitendea kazi vya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta katika uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Prof. Faustin Kamuzora.

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa katika uzinduzi wa bodi hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni