Alhamisi, 27 Oktoba 2016

WAZIRI MBARAWA APOKEA RIPOTI YA AWALI YA UPIMAJI WA MIPAKA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIA.


Mtaalam wa kurusha roboti ya ndege (Drone) kutoka Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) (Watatu kushoto), Bw. Fredrick Mbuya akitoa  ufafanuzi wa namna zoezi la kupiga picha katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) lilivyotekelezwa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa kwanza Kulia). Hatua hiyo itaiwezesha Serikali kumaliza mgogoro wa ardhi kati ya KIA na wananchi katika eneo hilo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, akikagua roboti ya ndege (Drone) iliyotumika katika zoezi la kupiga picha katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA). Kushoto ni Katibu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Vallery Chamulungu.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, akifatilia kwa makini maelezo ya Mtaalam wa kurusha roboti ya ndege (Drone) kutoka Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Fredrick Mbuya, wakati akipokea taarifa ya awali kuhusu zoezi la kupiga picha katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).


Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Hassan Mshinda akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ramani ya eneo la uwanja wa ndege wa KIA, baada ya zoezi la kupiga picha kukamilika.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni