|
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa mkandarasi
wa Kampuni ya Chongqing Foreign Trade and Economic Cooperation (Group) kutoka
China anayejenga barabara ya Tabora-Nyahua yenye urefu wa KM 85 alipokagua
kipande cha barabara ya Tabora mjini chenye urefu wa KM 6, mkoani Tabora.
|
|
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipokea taarifa ya maendeleo ya
mradi wa barabara ya Tabora-Nyahua kutoka kwa Meneja wa Wakala wa Barabara
nchini (TANROADS), mkoa wa Tabora Eng. Damian Ndabalinze, alipokagua kipande
cha barabara ya Tabora mjini chenye urefu wa KM 6.
|
|
Meneja wa Wakala wa
Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Tabora Eng. Damian Ndabalinze, akionesha
hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa barabara ya Tabora- Sikonge (Usesula) yenye
urefu wa KM 30 kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa.
|
|
Muonekano wa sehemu ya
barabara ya Tabora- Sikonge (Usesula) yenye urefu wa KM 30 ikiwa katika hatua
ya awali ya ujenzi wake.
|
|
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa mkandarasi
wa kampuni ya Chongqing International Construction Corporation (CICO), kutoka
China anayejenga barabara ya Tabora- Sikonge (Usesula) yenye urefu wa KM 30
alipokagua ujenzi wake.
|
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ametoa wiki mbili kwa
mkandarasi wa Kampuni ya Chongqing International Construction Corporation (CICO),
kutoka China anayejenga barabara ya Tabora- Sikonge (Usesula) yenye urefu wa
kilometa 30 kuongeza vifaa vya ujenzi katika eneo la mradi na
kuhakikisha ujenzi wake unatekelezwa kwa kasi na kukamilika kwa wakati.
Akizungumza
mara baada ya kukagua maendeleo ya mradi huo na kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji
wake Profesa Mbarawa amemtaka Mkandarasi huyo kutumia
kipindi cha muda wa ziada cha utekelezaji wa mradi huo kilichoongezwa
kukamilisha.
“Siridhishwi
na kasi unayoendelea nayo, kama hautatekeleza agizo hili haraka iwezekanavyo
nitasitisha mkataba huu mara moja na usitegemee kupata mradi mwingine wa
barabara nchini”, amesema Profesa Mbarawa.
Aidha,
Profesa Mbarawa amesema kuwa ujenzi wa mradi huo uende sambamba na
viwango bora vya barabara vilivyomo kwenye mkataba uliosainiwa.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mbarawa amekagua barabara ya Tabora – Nyahua yenye urefu
wa kilometa 85 kipande cha barabara ya Tabora mjini chenye urefu wa kilometa 6 kinachojengwa
na kampuni ya Chongqing Foreign Trade and Economic Cooperation (Group) kutoka
China na kumtaka mkandarasi kukamilisha barabara hiyo ifikapo mwezi Disemba
mwaka huu.
“Mpaka
mwezi Disemba nataka barabara hii iwe imekamilika kwa kiwango cha lami,
wananchi wa eneo hili wamekuwa
wakiisubiri kwa hamu, hivyo hakikisha unaikamilisha”, amesisitiza Prof Mbarawa.
Naye
Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Tabora Eng. Damian
Ndabalinze amesema kuwa wakala utamsimamia mkandarasi na kuhakikisha vifaa
vinaletwa katika eneo la mradi ndani ya mwezi huu.
Ameongeza
kuwa mradi huo unaenda sambamba na ujenzi wa madaraja makubwa mawili na
unagharimu zaidi ya Bilioni 28.
Kukamilika
kwa ujenzi wa miradi hiyo miwili kutafungua fursa nyingi ikiwa ni pamoja na
kurahisisha usafirishaji wa watu na bidhaa katika maeneo ya kati na Magharibi
mwa nchi yetu.
Waziri
Mbarawa yupo katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Tabora kukagua miundombinu ya barabara, uwanja wa
ndege, reli na mawasiliano.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni