Jumatano, 28 Septemba 2016

RAIS MAGUFULI AZINDUA RASMI NDEGE MPYA ZA BOMBARDIER


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akihutubia wananchi waliohudhuria uzinduzi wa ndege mbili mpya za Serikali zitakazoendeshwa na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) aina ya Bombardier Dash-8 Q400. Uzinduzi huo ulifanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Leonard Chamuriho akitoa taarifa katika uzinduzi wa ndege mbili mpya za Serikali zitakazoendeshwa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) aina ya Bombardier Dash-8 Q400. Uzinduzi huo ulifanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli.


Wajumbe wa Bodi a Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John  Pombe Magufuli (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa ndege mbili mpya za Serikali zitakazoendeshwa na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) aina ya Bombardier Dash-8 Q400.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akifafanua jambo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John  Pombe Magufuli katika hafla ya uzinduzi wa ndege mbili mpya za Serikali zitakazoendeshwa na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) aina ya Bombardier Dash-8 Q400.


Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi, Eng. John Kijazi (kushoto) akitiliana saini ya makabidhiano ya ndege mbili mpya za Serikali aina ya Bombardier Dash-8 Q400 zitakazoendeshwa na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Eng. Dkt. Leonard Chamuriho.


Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi, Eng. John Kijazi (kushoto) wakibadilishana hati za mkataba wa makabidhiano ya  ndege mbili za Serikali aina za Bombardier Dash-8 Q400 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya uchukuzi), Eng. Dkt. Leonard Chamuriho katika hafla ya uzinduzi wa ndege hizo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na viongozi wenzake mara baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa ndege mbili aina ya Bombardier Dash-8 Q400 zilizonunuliwa na Serikali.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John  Pombe Magufuli (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali walioshiriki hafla ya uzinduzi wa ndege mbili aina za Bombardier Dash-8 Q400 zilizonunuliwa na Serikali.