Katibu Mkuu wa Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (kulia),
akikagua daraja la Mwise lililopo katika barabara ya Bukoba- Mtukula.
|
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph
Nyamhanga ameuagiza uongozi wa
Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), na Wakala wa Majengo Nchini (TBA), mkoa
wa Kagera kufanya tathmini ya kina kwenye miundombinu ya barabara, madaraja na
majengo ya Serikali yalioathirika na tetemeko la ardhi.
Eng.
Nyamhanga ametoa agizo hilo Mkoani Kagera mara baada ya kukagua athari za
tetemeko la ardhi katika barabara za Bukoba- Mtukula, Kyaka-Bugene na jengo la
Kituo cha Pamoja cha Forodha cha Tanzania na Uganda ambapo amesema ni muhimu
kufanya utafiti wa kitaalam katika miundombinu hiyo kabla ya hatua za ukarabati
kuanza.
Amesema
kufanyika kwa utafiti huo utasaidia kubaini athari nyingine zilizojificha
ambazo zimetokana na tetemeko hilo.
“Undeni
kikosi kazi cha wataalam maramoja waweze kuchunguza ili kujua sehemu mbalimbali
zilizoathirika ili tuweze kuzitengeneza mapema iwezekanavyo”, amesema Eng.
Nyamhanga.
Katika
hatua nyingine Eng. Nyamhanga amemuagiza Mkandarasi wa Kampuni ya M/S China
Henan International Cooperation Group Co. Ltd (CHICO) inayojenga barabara ya
Kyaka-Bugeni (KM 59.1) kumaliza kipande cha Kilomita mbili katika barabara hiyo
ifikapo mwezi Disemba mwaka huu.
Amesema
kuwa kukamilika kwa kipande hicho kutaimarisha hali ya usafiri wa wananchi
katika wilaya za Bukoba na Karagwe na hivyo kuhuisha shughuli za kiuchumi kwa
wakazi wa Mkoa wa Kagera.
Eng. Nyamhanga yupo
mkoani Kagera kukagua athari za uharibifu wa miundombinu kufuatia tetemeko la
ardhi lililopiga mikoa ya Kagera, Mara na Mwanza Septemba 10 mwaka huu na
kusababisha vifo vya watu takribani 17, majeruhi zaidi ya 100, uharibifu wa
nyumba takribani 800 na miundombinu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni