|
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawsiliano Profesa Makame Mbarawa (Katikati), akitoa maelekezo kwa
Bodi mpya ya Shirika la ndege Tanzania (ATCL) wakati alipoitambulisha Bodi
hiyo, Jijini Dar es salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Eng. Edwin
Ngonyani na kushoto kwake ni Katibu Mkuu Eng. Leonard Chamriho.
|
Naibu Waziri wa Wizara
ya Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano, Eng.Edwin Ngonyani akifafanua jambo kwa
Wajumbe wa Bodi mpya ya Shirika la ndege Tanzania (ATCL) mara baada ya
kutangazwa kwake leo Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi
mpya ya Shrika la ndege Tanzania (ATCL), Emmanuel Korosso akitoa maelezo kwa Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawsiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) mara
baada ya kutambulishwa kwake leo jijini Dar es salaam.
|
Baadhi ya wajumbe wa
Bodi Mpya ya Shirika la ndege Tanzania (ATCL) wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) wakati wa
utambulisho wao leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ametoa miezi mitatu kwa Bodi
mpya ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kusuka upya uongozi uliopo ili
kuweza kuleta ufanisi wa utendaji kazi wa Shirika hilo.
Akizungumza jijini Dar
es salaam mara baada ya kuitambulisha Bodi hiyo, Waziri Mbarawa amesema kuwa Uteuzi
wa Bodi hiyo utasimamia kuleta tija na ufanisi wa shirika hilo ambalo kwa
kipindi kirefu lilikuwa na changamoto nyingi.
“Nataka kuona mabadiliko
makubwa kuanzia kwenye Menejimenti hadi uongozi wa chini, hakikisheni mnaweka
uongozi amabao utafuata maadili, utakuwa na ufanisi, ubunifu na kasi katika
utendaji kazi” amesema Profesa Mbarawa.
Aidha, ameitaka Bodi
hiyo kusimamia na kuboresha mpango wa kibiashara wa usafirishaji (Business
Plan) katika Shirika hilo ili kuweza kumudu soko la ushindani na kuweza
kuongeza mapato ya Shirika hilo.
“Kama mnavyojua
usafiri wa anga una ushindani mkubwa, hivyo ili Serikali iweze kupata faida
katika biashara hii ni lazima tuboreshe mpango wa kibiashara unaoendana na
wakati”, amesisistiza Waziri Mbarawa.
Profesa Mbarawa
ameitaka Bodi hiyo kuipa ATCL mifumo imara, makini na mahiri ili kuweza kutatua
changamoto zinazoikabili Shirika hilo ikwemo wizi wa mafuta ya ndege na upotevu
wa mapato.
Ili kupima ufanisi wa
utendaji wa Shirika hilo Profesa Mbarawa ameitaka Bodi hiyo kuandaa mkataba kwa
kila mfanyakazi kuanzia ngazi ya juu hadi chini.
Katika hatua nyingine
Waziri Mbarawa amesema kuwa Serikali ina mpango wa kununua ndege mbili mpya
aina ya Jet ifikapo mwaka 2017 kwa lengo la kuboresha sekta ya usafirishaji wa
anga nchini.
Kwa Upande wake, Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, ameitaka Bodi
hiyo kutumia fursa walioipata katika kufanya kazi vizuri ili kufufua shirika
hilo na kuwapatia watanzania huduma sahihi na bora za usafirishaji.
Naye, Mwenyekiti wa
Bodi hiyo Mhandisi Emmanuel Korosso, ameahidi kushirikiana na wajumbe wa bodi
yake katika kutekeleza maelekezo ya Waziri haraka iwezekanavyo ikiwemo
kubadilisha menejimenti ya shirika hilo.
| | | | | | |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni