Ndege ya kwanza ya Bombadier
Q400 iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL)
ikitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es
salaam
|
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kesho anatarajiwa kuzindua ndege
mbili mpya aina ya Bombardier Q 400 zilizonunuliwa na Serikali hivi karibuni.
Katibu Mkuu wa Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) Dkt. Leornard Chamuriho
amesema maandalizi yote kwa ajili ya uzinduzi wa ndege hizo yamekamilika na uzinduzi
huo utafanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)
kuanzia saa mbili asubuhi.
“Tunawaomba wanahabari
na wananchi kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi huo ili waone utekelezaji wa
ahadi wa Serikali katika mkakati wa kuhuisha usafiri wa Anga hapa nchini”,
amesema Dkt. Chamuriho.
Ndege hizo aina ya Bombardier
Q 400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja
zimetengenezwa nchini Canada na zitahudumia soko la ndani ndani na nchi
za jirani zitakapoanza kazi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni