Muonekano wa Barabara
wa Dodoma-Mayamaya yenye urefu wa KM 43.65 ikiwa katika hatua za mwisho za
ujenzi wake. Barabara hiyo inatarajiwa kukamilika mwezi Novemba Mwaka huu.
|
Muonekano wa tabaka la
kwanza la Barabara ya Dodoma-Mayamaya yenye urefu wa KM 43.65 ambayo ujenzi
wake unatarajiwa kukamilika mwezi Novemba mwaka huu.
|
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akiweka mchanga katika tabaka
la kwanza la ujenzi wa barabara ya Dodoma-Mayamaya yenye urefu wa KM 43.65
alipokagua mkoani Dodoma.
|
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akielekezwa namna ya
kushindilia mchanga katika barabara ya Dodoma-Mayamaya yenye urefu wa KM 43.65
mkoani Dodoma.
|
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemtaka Mkandarasi wa Kampuni
ya Ujenzi ya Sinohydro Corporation anayejenga barabara ya Dodoma-Mayamaya yenye
urefu wa kilometa 43.65 kukamilisha ujenzi huo ifikapo mwezi Novemba mwaka huu.
Akizungumza mara baada
ya kukagua barabara hiyo mkoani Dodoma na kuridhishwa na ujenzi wake Prof.
Mbarawa amesema kuwa barabara hiyo ni muhimu kwani ni kiungo kikuu kwa watu wanaosafiri kati ya mkoa
wa Dodoma, Manyara, Arusha na nchi za
Ukanda wa Kusini mwa Afrika.
“Kamilisheni kipande
hiki kilichobaki haraka kwani barabara hii ni kiunganishi cha nchi za Kaskazini
na Kusini mwa bara la Afrika hivyo kukamilika kwake kutasaidia kufungua fursa
za kibiashara na kukuza uchumi wa nchi”, amesema Waziri Mbarawa.
Amemtaka mkandarasi huyo kuzingatia viwango bora vya ujenzi wa barabara kama ilivyosainiwa kwenye mkataba na kuhakikisha thamani ya fedha katika ujenzi huo unaonekana.
Naye, Meneja wa Wakala
wa Barabara Nchini (TANROADS), Mkoa wa Dodoma Eng. Leonard Chimagu amemhakishia
Waziri huyo kusimamia barabara hiyo kwa mujibu wa sheria za barabara ikiwemo
kuzuia wananchi wasivamie miundombinu ya barabara na kuzuia mifugo kuswagwa
kwenye barabara.
“Nahakikisha
nitasimamia sheria za barabara, kwani mradi huu ni mkubwa na Serikali imetumia
gharama kubwa katika ujenzi wake, hivyo ni lazima niutunze ili kudumu muda
mrefu”, amefafanua Eng. Chimagu.
Barabara ya Dodoma – Mayamaya ni sehemu ya
mradi mzima wa barabara ya Dodoma – Babati yenye urefu wa kilometa 188.15 na
umegharimu shilingi bilioni 40.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni