WAZIRI PROF. MBARAWA AKAGUA MIUNDOMBINU MKOANI TABORA
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na mkandarasi wa Kampuni ya China Civil pamoja
na viongozi wa Serikali mkoani Tabora wakati akikagua ujenzi wa barabara ya
Ndono-Urambo yenye urefu wa KM 52 kuona hatua iliyofikiwa.
Meneja wa Wakala wa
Majengo Nchini (TBA), mkoa wa Tabora Qs.Tutu Lusama,akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kuhusu hatua iliyofikiwa ya
ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Urambo Bi Angelina Kwingwa wakati akikagua
ujenzi wake.
Muonekano wa Nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Urambo
mkoa wa Tabora, ambayo ipo kwenye hatua za mwisho za ujenzi wake
Mkandarasi wa Kampuni
ya Chicco kutoka China (kushoto), akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara ya Kaliua-Kazilambwa
yenye urefu wa KM 56 kwa Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa (kulia), alipokagua barabara hiyo kuona maendeleo yake.
Mbunge wa Jimbo la
Kaliua mkoani Tabora, Mhe. Magdalena Sakaya akifafanua jambo kwa Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa wakati alipokagua
barabara ya Kaliua-Kazilambwa yenye urefu wa KM 56 kuona maendeleo yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni