Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akifafanua jambo kwa wakazi
wa kata ya Mpata wakati alipokagua miundombinu ya barabara katika kata hiyo.
|
Wakazi wa mwakaleli wakimsikiliza
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (hayupo
pichani).
|
Serikali imesema
itaijenga kwa kiwango cha lami barabara ya Katumba-Mbambo hadi Tukuyu KM 79.4
ili kuiunganisha kwa lami wilaya mpya ya Busekelo na Wilaya nyingine za mkoa wa
Mbeya na hivyo kukuza uchumi wa wilaya hiyo.
Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng.Edwin Ngonyani amesema hayo mara baada ya
kukagua ujenzi wa barabara hiyo unaendelea katika sehemu ya Lupaso hadi Bujesi
KM 10 na kumtaka mkandarasi anayejenga barabara hiyo kampuni ya Chongqing
International Construction Corporation (CICO)
kuongeza kasi ya ujenzi huo kwa kuzingatia makubaliano yaliyopo kwenye mkataba.
“Nawaomba wananchi wa
Busokelo msimcheleweshe mkandarasi kufanya kazi yake kwa kuepuka vitendo
vinavyoweza kuchelewesha ujenzi wa barabara hii kwa kufungua kesi za kudai
fidia kwani kwa kufanya hivyo kunachelewesha maaendeleo ya ujenzi wa barabara
hii”. amesema Eng. Ngonyani.
Eng. Ngonyani amewataka wananchi wa Wilaya ya Busokelo kushirikina na viongozi wao na kutoa ushirikiano unaostahili ili kasi ya ujenzi wa baraba za lami katika maeneo yao isikwamishwe na wananchi wachache.
Akiwa wilayani Busekelo Naibu Waziri huyo amekagua barabara za Kata ya Mpata na Luteba ambazo zinasimamiwa na halmashauri na kuahaidi kushirikiana na Wizara nyingine ili kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara katika wilaya hiyo inayozalisha mazao mengi chakula na biashara yanayosafirishwa katika miji mikubwa nchini.
Naibu Waziri Ngonyani
amezungumzia umuhimu wa kuziunganisha wilaya za Makete na Busokelo kwa lami ili
kurahisisha usafirishaji wa mazao na kukuza utalii katika hifadhi ya kitulo.
Amemuagiza Meneja wa
wakala wa barabara (TANROADS) mkoa wa Mbeya Eng. Paul Lyakurwa kushirikiana na
halmashauri ya Busokelo katika baadhi ya miradi ili kuongeza kasi ya kuboresha
barabara na hivyo kuhuisha uchumi wa wakazi wa wilaya hiyo.
Naye Mbunge wa
Busokelo Mhe. Atupele Mwakibete amemuomba Naibu waziri Ngonyani kuangalia namna
ya kuijenga barabara ya Kata ya Mpata ili kuwezesha magari mengi
yanayosafirisha gesi kufika kwa urahisi katika eneo hilo na hivyo kurahisha
usafirishaji wa gesi,kuongeza ajira kwa vijana na kuongeza pato la halmashauri
hiyo.
“Mhe. Waziri wananchi
wa Mpata na Luteba wako tayari kutoa maeneo yao bila fidia ili barabara ijengwe katika eneo hilo ambalo
ni muhimu kwa uzalishaji wa viazi na ndizi”. Amesistiza Mwakibete.
Naibu waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonuani yupo katika ziara mikoani ya
nyanda za juu kusini kukagua miradi ya ujenzi na kutoa maelekezo kwa taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni