Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akikagua Meli ya
Mv. Njombe ambayo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99.
|
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akikagua mfumo wa
uendeshaji wa Meli ya Mv. Njombe ambao ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 99.
|
Muonekano
wa Meli za Mv. Njombe na Mv.Ruvuma ambazo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia
99, meli hizo zipo katiaka hatua za majaribio kabla ya kuanza kutoa huduma.
|
Imeelezwa
kuwa uchumi wa wananchi wa Mikoa ya Njombe, Mbeya na Ruvuma utaimarika kwa kasi
kama watatumia vizuri fursa ya uwepo wa meli za mizigo na abiria katika ziwa
Nyasa.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani amesema kukamilika kwa meli mbili za mizigo za Mv. Njombe na Mv. Ruvuma na ujenzi wa meli ya abiria ya Mv. Mbeya ni fursa mpya ya kiuchumi kwa wakazi wa mikoa hiyo.
“Tumejipanga
kuhakikisha tunafungua ukanda huu wa nyanda za juu kusini kiuchumi hivyo ni
jukumu la wananchi kuchangamkia fursa za kibiashara zinazoweza kusafirishwa
ndani na nje ya nchi ili kukuza uchumi”.amesema Eng. Ngonyani.
Naibu
Waziri Ngonyani ameelezea kuridhishwa kwake na hatua ya ujenzi wa meli za Mv.Njombe
na Ruvuma ambao umefikia asilimia tisini na tisa na kusisitiza kuwa Serikali itaendelea
kuwaamini makandarasi wazawa wanaofanya kazi kwa ubunifu, uadilifu na uaminifu
ili kutoa fursa nyingi za ajira kwa watanzania.
Kaimu
Meneja wa bandari ya Itungi na Kiwira Eng. Juma Kisavara amemhakikishia Naibu Waziri
Ngonyani kuwa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) imejipanga kuhaikikisha bandari
zote kumi na tano zilizopo katika ziwa Nyasa kwa upande wa Tanzania
zinafufuliwa na kutumika kupakia na kushusha mizigi ikiwemo vifaa vya ujenzi,
makaa ya mawe,mbolea na mazao ambayo yana soko ndani na nchi za jirani.
Eng.
Kisavara amemhakishia Naibu wa Ujenzi kuwa tayari wametafuta soko la kutosha la
kusafirisha mizigo hivyo kuiomba Serikali kuendelea na kasi ya ujenzi wa meli
nyingine zitakazotumika katika ziwa Nyasa.
Zaidi
ya shilingi bilioni 11 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa Meli ya Mv.Ruvuma na
Mv. Njombe zinazojengwa na kampuni ya Songoro Marine Transport ya hapa nchini
na meli hizo zinatarajiwa kukabidhiwa kwa Serikali mwezi Januari mwakani.
Katika
hatua nyingine Naibu Waziri Ngonyani amekagua ujenzi wa barabara ya
Kikusya-Ipinda hadi Matema KM 34.6 wilayani Kyela inayojengwa kwa kiwango cha
lami na kusisitiza kuwa Serikali italipa fedha kwa mkandarasi anayejenga barabara
hiyo ili kuiwezesha kukamilika kwa muda uliopangwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni