Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa
Menejimenti na Wafanyakazi wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), katika mkutano
uliofanyika jijini Dar es Salaam.
|
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akimpongeza mmoja wa
watoa huduma wa ndege za ATCL kwa utoaji wa huduma bora kwa wateja katika
mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam.
|
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ametoa muda wa mwezi
mmoja kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kufanya
mabadiliko katika menejimenti ya Shirika hilo ili kuongeza ufanisi na kuboresha
utendaji kazi.
Ametoa
agizo hilo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza katika mkutano wa
Menejimenti pamoja na wafanyakazi wa Shirika hilo na kuwataka kutoa huduma bora
ili kulifanya Shirika hilo kuwa miongoni mwa mashirika bora ya ndege barani Afrika.
“Nataka
ndani ya mwezi mmoja uwe umeshafanya mabadiliko katika menejimenti, mabadiliko
lazima yaanzie juu kwanza kwa watoa maamuzi na ishuke hadi kwa wafanyakazi
wazembe na wasio waadilifu”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Waziri
Mbarawa amepinga nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi wa Shirika hilo hasa
katika kipindi hiki ambacho Serikali ipo katika juhudi za kulifufua na
kuliimarisha Shirika hilo.
Aidha
Waziri Mbarawa ameitaka Idara ya Masoko ya shirika hilo kuzunguka katika
taasisi zote zilizo chini ya Wizara yake na kuzishawishi kuweza kutumia huduma
za usafiri wa anga wa ATCL.
“Serikali
imekamilisha upande wake wa ununuzi wa ndege, sasa kazi inabaki kwenu, sitaki
watu wa masoko kukaa ofisini”, amesema Prof. Mbarawa.
Ameongeza
kuwa wafanyakazi wa ATC wanatakiwa kujipanga kutoa huduma iliyotukuka kwa
wateja wake ili kuweza kuhimili ushindani uliopo katika mashirika ya ndege
nchini.
“Inabidi
tofauti kubwa ionekane kati yenu na mashirika mengine, yeyote ambaye anaona
hawezi kutoa huduma bora kwa mteja atafute sehemu nyingine kwani hapa hatufai ”,
amesisitiza Waziri Mbarawa.
Profesa
Mbarawa amelitaka shirika hilo kutumia mfumo wa kisasa wa kukata tiketi kwa
njia ya simu na kompyuta ili kuwarahishia watumiaji wa shirika hilo kuweza
kupata tiketi kwa haraka na urahisi.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Eng. Ladislaus Matindi
amemhakikishia Waziri Mbarawa kufanyia kazi maagizo aliyotoa na kuahidi kuboresha
utendaji kazi wa shirika hilo kwa lengo
la kuteka soko la ushindani wa usafiri wa anga nchini.
“Kwa
sasa tumeanza vizuri na naamini uwezo wa kuzalisha faida zaidi tunao, tunaahidi
kuboresha utendaji kazi ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya Serikali ya Awamu
ya Tano”, amesema Eng. Matindi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni