Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli katika mkutano wa kimataifa wa Usafirishaji Duniani
utakaofanyika katika mji wa Ashgabat nchini Turkemistan kuanzia tarehe 26-27
Novemba, 2016.
Ajenda kuu ya mkutano huo ulioitishwa na
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambao utashirikisha viongozi mbalimbali utajadili
kwa kina maeneo muhimu ya ushirikiano wa kimataifa kwenye Sekta ya Usafirishaji
kwa maendeleo endelevu Duniani.
Aidha katika mkutano huo Waziri Prof. Mbarawa atapata
fursa ya kukutana na wawekezaji mbalimbali Duniani waliobobea katika sekta ya
usafirishaji na kuwashawishi kuwekeza hapa nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni