Wananchi
hao wamemweleza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin
Ngonyani, alipofika kukagua daraja hilo mkoani humo jana, ambapo pamoja na
mambo mengine wamesema kuwa kukamilika kwa daraja hilo kutatatua changamoto za
usafiri hususan katika kipindi cha masika.
"Tunaomba
Mheshimiwa Naibu Waziri utusaidie kukamilisha daraja hili mapema
ili tupate huduma muhimu kama usafiri hasa kipindi cha masika",
amesema mmoja wa wananchi.
Aidha,
wananchi hao wameipongeza Serikali kwa kuendelea na jitahada za ujenzi wa
barabara za maingilio zenye urefu wa KM 25 katika daraja hilo ambapo kwa sasa mradi
wote umefika asilimia 43.9.
Kwa
upande wake Naibu Waziri Eng. Ngonyani ameuagiza Uongozi wa Wakala wa Barabara
nchini (TANROADS), mkoani humo kuhakikisha kuwa wanamsimamia mkandarasi na kuhakikisha
anamaliza ujenzi wa daraja hilo pamoja na barabara hizo kufikia mwezi Machi
mwakani.
Kuhusu
deni la mkandarasi huyo analoidai Serikali, Eng. Ngonyani amesema kuwa
watahakikisha wanamlipa mapema ili kufanikisha mradi kumalizika kwa muda
uliopangwa.
"Tutahakikisha
tunalipa deni lote linalodaiwa ili kurahisisha mradi huu kuisha haraka kwa
ajili ya wananchi kuweza kutumia daraja hili pamoja na barabara yake kwa kuwa
ni kiungo muhimu kwao", amesisitiza Naibu Waziri.
Ametoa
rai kwa wananchi wa maeneo hayo mara tu mradi unapomalizika kuhakikisha
wanalinda miundombinu yake kwani Serikali inatumia gharama kubwa katika
utekelezaji wake.
Naye,
Kaimu Meneja wa TANROADS mkoani humo, Eng. Yohanes Mbegalo, amemuahidi
Naibu Waziri huyo kuwa atahakikisha mradi huo unaisha kwa wakati ili
kuwaondolea wananchi kero ya usafiri.
Daraja
la Sibiti lenye urefu wa mita 82 linajengwa na mkandarasi China Hanan ambalo
linatarajiwa kukamilika mwezi Machi mwakani na kugharimu zaidi ya shilingi
bilioni 16.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni