|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikaribishwa na Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa katika moja ya banda
lililopo katika ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Kikwete kabla ya kufungua
Mkutano wa 20 wa Mashauriano ya Bodi ya Makandarasi (CRB), uliofanyika mjini
Dodoma.
|
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia), akikabidhiwa zawadi na
mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Denim Eleveators (kushoto) baada ya kukagua
banda hilo katika ufunguzi wa Mkutano wa 20 wa Mashauriano ya Bodi ya
Makandarasi (CRB), uliofanyika mjini Dodoma.
|
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakiwa katika ufunguzi wa Mkutano wa 20 wa
Mashauriano ya Bodi ya Makandarasi (CRB), uliofanyika mjini Dodoma.
|
|
Msajili wa Bodi ya Makandarasi
Eng. Reuben Nkori akitoa taarifa ya kiutendaji kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa
20 wa Mashauriano ya Bodi ya Makandarasi (CRB), uliofanyika mjini Dodoma.
|
|
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na Makandarasi
waliohudhuria Mkutano wa Mashauriano ya
Bodi ya Makandarasi (CRB), wenye kauli mbiu “Miaka 20 ya CRB Utendaji wa Makandarasi unaozingatia maadili na sheria
kama mkakati wa kuaminiwa na waajiri”, uliofanyika mjini Dodoma.
|
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Makandarasi
waliohudhuria Mkutano wa Mashauriano ya Bodi ya Makandarasi (CRB), wenye kauli
mbiu “Miaka 20 ya CRB Utendaji wa
Makandarasi unaozingatia maadili na sheria kama mkakati wa kuaminiwa na waajiri”,
uliofanyika mjini Dodoma.
|
|
Makandarasi wakisikiliza hotuba
ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati
wa ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano ya Bodi ya Makandarasi (CRB), wenye kauli
mbiu “Miaka 20 ya CRB Utendaji wa
Makandarasi unaozingatia maadili na sheria kama mkakati wa kuaminiwa na
waajiri”, uliofanyika mjini Dodoma.
|
|
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana (kushoto), wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 20 wa Mashauriano
ya Bodi ya Makandarasi (CRB), uliofanyika mjini Dodoma.
|
Mwakilishi kutoka Wakala wa
Barabara Nchini (TANROADS), akipokea tuzo kutoka kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa ufunguzi wa Mkutano
wa 20 wa Mashauriano ya Bodi ya Makandarasi (CRB), uliofanyika mjini Dodoma.
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na
Watendaji wa Bodi ya Usajili ya Makandarasi (CRB), na viongozi wengine wa
Wizara katika ufunguzi wa Mkutano wa 20 wa mwaka wa CRB, uliofanyika mjini Dodoma.
Serikali imewataka
Makandarasi kuwajibika na kufanya kazi zao kwa ufanisi na weledi ili
kuishawishi Serikali kuwaamini na kuwapatia zabuni za kutekeleza miradi mikubwa
nchini.
Akizungumza katika ufunguzi
wa Mkutano wa 20 wa Mashauriano ya Bodi ya Makandarasi (CRB), mjini Dodoma,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,
amesema kuwa miradi mingi mikubwa nchini imekuwa ikitekelezwa na Makandarasi
kutoka nje ya nchi hali inayopelekea Serikali kutumia fedha nyingi kuwalipa
Makandarasi hao.
“Muda umefika sasa kwa
makandarasi wazawa kuungana na kuomba zabuni za kutekeleza miradi mikubwa
itakayowajengea uwezo kama ujenzi wa bomba la Mafuta kutoka Uganda hadi Tanga,
Reli ya Kisasa na miradi mingine”, amesema Makamu wa Rais.
Aidha, amefafanua kuwa
kutekelezwa kwa miradi hiyo na Makandarasi wazawa kutaokoa fedha za ndani za watanzania na hivyo kupelekea fedha hizo
kubaki nchini na vijana kupata ajira.
Sambamba na hilo
Makamu wa Rais amewasisitiza Makandarasi hao kuwa wa kwanza kuomba zabuni pindi zinapotangazwa kwani Serikali
ya Awamu ya Tano itatoa kipaumbele kwa Makandarasi wazawa wote nchini.
Makamu wa Rais ameitaka
CRB kuhakikisha inasimamia Makandarasi hao kutekeleza miradi kwa muda
uliopangwa pamoja na kufuata maadili katika utendaji wao wa kazi.
Kuhusu suala la
ulipaji wa madeni ya Makandarasi Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa kwa sasa Serikali inendelea kufanya
uhakiki wa madeni hayo ambapo zoezi la malipo litaanza mara baada ya uhakiki
huo kukamilika.
Kwa Upande wake,
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa
kutokana na umuhimu wa kuwathamini Makandarasi wazawa Wizara imetenga miradi
maalum kwa ajili ya kuwajengea uwezo Makandarasi hao.
Profesa Mbarawa amewahakikishia
makandarasi hao kupata fursa kwa zabuni zinazotangazwa na Wizara kwa kila
Mkandarasi mwenye sifa atakayeomba zabuni hizo.
“Makandarasi msisite
kuomba zabuni pindi zinapotangazwa, naahidi nitasimamia kwa uaminifu na kuhakikisha
kila mkandarasi mwenye sifa anapata zabuni kwa mujibu wa sheria”, amesema
Profesa Mbarawa.
Naye, Mwenyekiti wa
Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini, Eng. Consolata Ngimbwa amemhakikishia
Makamu wa Rais kuwa watatumia mkutano huo kujadili changamoto zinazowakabili na
hivyo kuja na mapendekezo sahihi ya kutatua changemoto hizo.
Mkutano huo wa siku
mbili wenye kauli mbiu isemayo “Miaka 20
ya CRB, utendaji wa Makandarasi unaozingatia maadili na Sheria kama mkakati wa
kuaminiwa na waajiri” una lengo la
kuwakutanisha makandarasi wa ndani na
nje ya nchi kwa lengo la kujadili kwa pamoja changamoto zao na kuzitafutia
ufumbuzi.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni