Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akipokea taarifa ya
maendeleo kutoka kwa Mhandisi Mkazi Eng. Juma Msonge (Wa tatu kulia), kuhusu ujenzi wa barabara
ya Uyovu-Bwanga KM 45 inayojengwa kwa kiwango cha lami wakati alipokagua
barabara hiyo jana, mkoani Geita
|
Mhandisi Mkazi Eng.
Juma Msonge, akitoa taarifa ya maendeleo yaliyofikiwa ya ujenzi wa barabara ya
Uyovu-Bwanga KM 45 inayojengwa kwa kiwango cha lami jana, mkoani Geita kwa
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa pili kulia).
|
Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, akitoa maelekezo kwa
Mhadisi Mkazi Eng. Juma Msonge, baada ya kukagua ujenzi wa barabara ya
Uyovu-Bwanga KM 45 inayojengwa kwa kiwango cha lami jana, mkoani Geita.
|
Meneja wa Wakala wa
Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Geita, Eng. Harun Senkuku, akifafanua jambo
kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani, ambae
alikuwa mkoani humo kwa ajili ya kukagua miradi inayotekelezwa na Wizara yake.
|
|
Sehemu ya barabara ya
Uyovu-Bwanga KM 45 inayojengwa kwa kiwango cha lami na Mkandarasi Synohdro, mkoani
Geita. Hadi sasa ujenzi wake umefikia asilimia 60.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani ameridhishwa na
kasi ya ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga yenye urefu wa Km 45 inayojengwa na
Mkandarasi M/S Sinohydro Corporation.
Akizungumza
mkoani Geita jana, mara baada ya kukagua barabara hiyo ikiwa ni sehemu ya
mradi wa ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga-Biharamulo KM 112, Naibu Waziri
Eng. Ngonyani amemtaka mkandarasi huyo kahakikisha wanamaliza sehemu iliyobakia
kwa muda uliopangwa.
"Nimeridhishwa
na kasi yenu, hakika mmepiga hatua sana kwani awali nilipopita kukagua barabara
hii haikuwa hivi", amesema Naibu Waziri Ngonyani.
Aidha,
Eng. Ngonyani, amewapongeza wasimamizi wa barabara ya Biharamulo - Bwanga
kutoka wakala wa barabara nchini (TANROADS) kupitia kitengo chake maalum cha
wahandisi washauri wazawa (TECU), kwa kuhakikisha wanamsimamia mkandarasi
M/S Sinohydro Corporation kujenga barabara hiyo kwa viwango vilivyomo
kwenye mkataba.
Kwa
upande wake, Mhandisi mkazi wa barabara hiyo Eng. Juma Msonge, amemhakikishia
Waziri huyo kumaliza barabara hiyo kwa wakati.
Eng.
Msonge ameongeza kuwa kwa sasa mradi huo umefika asilimia 60 ambapo mkandarasi
anaendelea na kazi ya kuweka matabaka ya lami ambapo ameshaweka km 30 kati ya
45 zilizopo kwenye barabara hiyo.
Naibu Waziri Ngonyani, amemaliza ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Geita
ambapo pamoja na mambo mengine ametembelea na kukagua miradi mbalimbali
inayotekelezwa na Wizara yake.
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni