Wafanyakazi wa Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), wakiwa katika picha ya
pamoja mara baada ya kufunga kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika
Mkoani Morogoro.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng.Joseph
Nyamhanga, amewataka watumishi wa Wizara hiyo kutekeleza majukumu yao kwa
weledi na uadilifu ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya Serikali ya Awamu ya
Tano.
Akisoma
hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Profesa Makame Mbarawa,
katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi leo, mkoani Morogoro, Eng. Nyamhanga,
ametoa wito kwa watumishi wote kushirikiana kwa pamoja katika kutekeleza
majukumu yao ili kuleta tija kwa Serikali na Taifa kwa ujumla.
"Naliomba
baraza hili la wafanyakazi kuhakikisha linahamasisha watumishi wote wa Wizara
kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili, weledi na ushirikiano ili
kuleta ufanisi", amesema Eng.Nyamhanga.
Aidha,
Eng. Nyamhanga amelisisitiza Baraza hilo kuandaa mkataba wa kupima utendaji
kazi wa watumishi katika majukumu yao ya kila siku ili kupima ufanisi wa
watumishi hao kuanzia ngazi ya juu hadi ya chini.
Katibu
Mkuu Nyamhanga, amelitaka Baraza hilo kuweka mazingira maalum kwa
watumishi ikiwemo kuandaa mpango wa mafunzo ya ndani na nje ya nchi ili
kuongeza ujuzi kwa watumishi wa Wizara hiyo.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Tawi la Ujenzi Bw. Samuel
Mticco, amemhakikishia Katibu Mkuu huyo kutekeleza maagizo yote
yaliyosemwa katika Baraza hilo ikiwemo la uandaaji wa mkataba wa utendaji
kazi kwa watumishi.
Kikao hicho cha siku moja
cha Baraza la wafanyakazi la Sekta ya Ujenzi pamoja na mambo mengine
kimekubaliana kupunguza matumizi ya fedha za Serikali yasiyo ya lazima pamoja
na kupambana na vitendo vya ufisadi na rushwa
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni