Waziri
wa Ujenzi, Uchukukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (Mb), kwa
mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali Na. 30 ya mwaka
1997 pamoja na marekebisho yake kupitia Sheria Na. 13 ya mwaka 2009 amemteua
Dkt. Edward Wilson Ngwale kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa
Majengo Tanzania (TBA) kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 10.04.2017.
Mhe.
Prof. Mbarawa amemteua Dkt. Ngwale kushika nafasi hiyo kwa kipindi kingine cha
miaka mitatu katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi baada ya uteuzi wa awali kufika
ukomo.
Aidha,
sambamba na uteuzi huo Prof. Mbarawa amewateua Wajumbe watano (5) wa Bodi ya
Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania kuanzia tarehe 10.04.2017 kama
ifuatavyo:-
1. Eng.
John Bura – Mkandarasi kupitia Bodi ya
Usajili wa Makandarasi (CRB)
2. Arch. Pius P. Tesha – Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
3. Prof. Bakari M. M. Mwinyiwiwa – Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
4. Bw. Ntuli Lutengano Mwakahesya – Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
5. Eng. Amiri N. Mcharo – Wizara ya Fedha na Mipango.

Imetolewa
na;
Eng.
Joseph M. Nyamhanga
KATIBU
MKUU (UJENZI)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni