Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (mwenye suti),
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), mara baada ya kukagua
kichwa cha treni ambacho kilikuwa kikifanyiwa ukarabati katika karakana ya
TAZARA mkoani Mbeya. Kushoto kwake ni Meneja wa TAZARA mkoa wa Tanzania Bw. Fuad
Abdallah.
Serikali
imeipongeza Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), kwa kutekeleza agizo
la kukamilisha ukarabati wa kichwa cha Treni ndani ya miezi miwili ambacho
kilikuwa kikifanyiwa ukarabati wake katika
karakana ya Mbeya.
Akiongea
mara baada ya kukikagua kichwa hicho katika karakana ya Mamlaka hiyo jijini Dar
es salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
amesema kukamilika kwake kutasaidia huduma bora na ya uhakika kwa usafirishaji
wa mizigo na abiria.
“Nimefurahishwa
na uharaka wenu wa utendaji kazi, kwani nilitoa miezi miwili kwa TAZARA
kukarabati kichwa hiki haraka
iwezekanavyo kutokana na umuhimu wake”, amesema Waziri Mbarawa.
Aidha,
Profesa Mbarawa ametoa wito kwa wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kufanya kazi kwa
moyo na kwa ufanisi ili kuweza kufufua Mamlaka hiyo ambapo kwa kipindi kirefu
ilikuwa na misukosuko mingi.
Naye
Meneja wa TAZARA mkoa wa Tanzania Bw. Fuad Abdallah, amemuhakikishia Waziri Prof.
Mbarawa kuwa Mamlaka hiyo itaendelea na huduma za usafirishaji wa mizigo na
abiria ndani na nje ya nchi.
“Kwa
sasa TAZARA inaendelea kuboresha na kuimarisha huduma za usafirishaji wa mizigo
kutoka Bandari ya Dar es salaam hadi New Kapiri Mposhi kati ya siku nne hadi saba
ukilinganisha na siku zilizopita”, amesema Bw. Fuad.
Kichwa
hicho cha Treni kimekarabatiwa kwa gharama ya shilingi Bilioni moja ambapo
Serikali imeokoa Bilioni Tisa mpaka Kumi endapo ingenunua kichwa kipya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni