Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli alipohutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza. |
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli ameitaka Wizara
ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano kuhakikisha kuwa ujenzi wa daraja la watembea
kwa miguu na upanuzi wa Barabara ya Makongoro jijini Mwanza unakamilika ifikapo
disemba mwaka huu.
Aidha
amesema upanuzi wa barabara ya Makongoro uliokuwa ujengwe kati ya Furahisha hadi
Pasiansi Km 2.8 sasa utaendelezwa hadi kufikia uwanja wa ndege.
Akizungumza
mara baada ya kuweka jiwe la msingi la daraja la watembea kwa miguu na upanuzi
wa barabara ya Makongoro Mh. Dkt. Magufuli amesema kasi ya ujenzi wa barabara
jijini Mwanza uendane na ujenzi wa uwanja wa ndege ili kuwezesha mkoa wa Mwanza
kuwa kitovu cha nchi za maziwa makuu.
“Nakuagiza
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano
uhakikishe kuwa barabara na daraja la watembea kwa miguu Furahisha
vinakamilika mwezi desemba na mkandarasi wa uwanja wa ndege anaanza kazi mara
moja”. Amesisitiza Rais Dkt. Magufuli.
Amesema
nia ya Serikali yake ni kununua meli mbili na kujenga daraja kati ya Kigongo na
Busisi ili kuboresha huduma za usafiri katika Ziwa Victoria.
Naye
Mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale amemtaka
mkandarasi anaejenga daraja la waenda kwa miguu na barabara ya Makongoro kuhakikisha
ujenzi wake unakamilika kwa wakati na ubora unaotakiwa.
Zaidi
ya shilingi bilioni 6.4 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi huo utakaopunguza
msongamano wa magari na ajali katika barabara ya makongoro jijini Mwanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni