Waziri wa Ujenzi Uchukuzi
na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa amewataka wafanyakazi wote katika
sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kufanya kazi kwa uadilifu na
ushirikiano katika kuwahudumia watanzania ili kufikia malengo ya Wizara.
Prof. Mbarawa
ameyasema hayo jana katika mapokezi ya Manaibu Mawaziri wapya wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Jijini Dar Es Salaam baada ya kuapishwa na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu Dar es
Salaam.
“Mimi nafurahi sana
kufanya kazi katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa sababu mimi
na wafanyakazi tuko katika timu moja; tunafanya kazi kwa pamoja na kwa ushirikiano.
Katika kipindi cha miaka miwili tumefanikiwa kufikia malengo mbalimbali ya
serikali mfano ujenzi wa reli ya kisasa na barabara “ Mhe. Mbarawa amesema.
Akiwakaribisha Manaibu Mawaziri hao katika
Wizara hiyo Prof. Mbarawa amesema yeye pamoja na wafanyakazi wote wa wizara wamefurahi
kupata mawaziri wapya ambao watafanya nao kazi kwa pamoja katika wizara hiyo.
“Sisi kama viongozi tunapaswa kuwa mfano
katika utendaji wetu wa kazi ili kujenga imani na umoja na wafanyakazi wetu, tunapaswa kufanya kazi kwa uadilifu, ushirikiano na umoja kwani haya ndio
masuala ya msingi katika utendaji kazi,” Prof. Mbarawa amesema.
Kwa upande wake Naibu
Waziri anayeshughulikia Sekta ya
Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Atashasta Nditiye amesema kuwa amejipanga kufanya kazi na kuleta matokeo
chanya kwa maendeleo ya nchi.
“Nipo tayari kufanya
kazi itakayoleta mabadiliko, tutaboresha miundombinu ili kuchochea kasi ya
ukuaji wa viwanda ,” amesema mhandisi Nditiye.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anaesimamia Sekta ya Ujenzi, Mhe. Elias Kwandikwa amesema atahakikisha anatumia vipaji vyake vyote katika kujenga umoja, uadilifu ili kufikia malengo ya sekta ya ujenzi.
|
Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Atashasta Nditiye (Wa pili kulia) akisalimiana
na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eng. Joseph Nyamhanga (Kushoto) wakati
alipokaribishwa katika ofisi za Wizara leo Jijini Dar es Salaam, Kulia ni
Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho na Wa pili kushoto Katibu
Mkuu Dkt. Maria Sasabo (Sekta ya Mawasiliano).
|
|
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawailiano, Prof. Makame Mbarawa (Kushoto), akisalimiana na Naibu
Waziri Eng. Atashasta Nditiye (Kulia), wakati alipomtembelea Waziri Mbarawa
ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Katibu Mkuu Sekta ya
Uchukuzi Dkt Leonard Chamuriho
|
|
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawailiano, Profesa Makame Mbarawa (Kulia) akisalimiana na Naibu
Waziri hiyo Mhe. Elias Kwandikwa wakati alipomtembelea Waziri Mbarawa ofisini
kwake leo Jijini Dar es Salaam.
|
|
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (Katikati) akizungumza na Manaibu
Waziri wa Wizara hiyo Eng. Atashasta Nditiye (Wa pili kulia) na Mhe. Elias
Kwandikwa (Wa tatu kulia), wakati walipomtembelea ofisini kwake Jijini Dar
es Salaam,
|
|
Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Atashasta Nditiye (aliyesimama) akifafanua
jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (Wa
kwanza kulia), mara baada ya kuapishwa Jijini Dar es Salaam.
|
|
Naibu Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Elias Kwandikwa (aliyesimama) akieleza
jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Prof. Makame Mbarawa (Wa
kwanza kulia), leo Jijini Dar es Salaam kabla ya kikao kazi na Makatibu Wakuu
wa wizara na baadhi ya Watendaji waliopo jiji Dar es Salaam.
|
|
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano,
Profesa Makame Mbarawa (Kulia) akiwakabidhi manaibu Waziri wa Wizara hiyo Eng.
Atashasta Nditiye (Kulia) na Mhe. Elias Kwandikwa wakati (Katikati) vitabu vya
bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18 ya Wizara hiyo kama mwongozo wa utendaji kazi
mara baada ya kuapishwa jijini Dar es Salaam |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni