Ijumaa, 7 Oktoba 2016

TANROADS YAAGIZWA KUBORESHA UTENDAJI


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wajumbe katika Baraza la Saba la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), lililofanyika mkoani Dodoma.


Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Saba la Wafanyakazi akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Wakala huo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani). Baraza hilo limefanyika mkoani Dodoma.


Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Saba la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani), katika Baraza hilo.


Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa katika Baraza la Saba la Wafanyakazi wa Wakala huo lililofanyika mkoani Dodoma.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Saba la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS).


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akimsikiliza mmoja wa wajumbe waliohudhuria katika Baraza la Saba la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoani Dodoma.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameuagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuboresha Idara ya Mipango na Usanifu katika wakala huo ili kupata matokeo mazuri katika utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini.


Prof. Mbarawa ameutaka wakala huo kuboresha kanuni zinazosimamia aina ya vyombo vya moto vinavyotumia barabara zote nchini ili kuweza kusaidia miundombinu hiyo kudumu muda mrefu.Akizungumza mkoani Dodoma katika ufunguzi wa Baraza la Saba la Wafanyakazi wa Wakala huo Prof. Mbarawa amesema kuwa wakala unabidi uanze kubadili aina ya mfumo wa usanifu uliokuwa ukitumika awali na badala yake utumike usanifu wa kisasa unaoendana na mahitaji halisi ya watumiaji wa barabara hizo.

“Kama mnaona kuna mabadiliko yoyote mnayohitaji kuyafanya ili barabara zetu zidumu, boresheni kanuni na mlete kwangu ili nizifanyie kazi”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Ameongeza kuwa katika kuboresha utendaji katika wakala huo, Serikali ina mpango wa kuwapa fursa za ajira wahandisi hususani wanawake na kuwajengea uwezo na kuweka uwiano katika taalamu hiyo.

Aidha Waziri Prof. Mbarawa ameahidi kuongeza fedha za uendeshaji kwa wakala huo ili kuuwezesha kutekeleza miradi mbalimbali inayoendelea nchini.

“Kumbukeni majukumu ya Wakala yameongezeka sasa hamtajenga barabara pekee, mmeongezewa jukumu la kujenga miundombinu ya viwanja vya ndege hivyo ni muhimu kujipanga kutekeleza kazi hii”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

Naye, Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Eng. Patrick Mfugale ameahidi kushughulikia ujenzi wa viwanja vya ndege ikiwemo kufanya kazi kwa weledi na uadilifu kama ambavyo wakala huo unatekeleza miradi yake ya barabara.

Ameongeza kuwa Wakala unaendelea kufanya kazi na Makandarasi wenye uwezo na wanaozingatia thamani ya fedha katika miradi yote inayotekelezwa nchini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TANROADS, Eng. Hawa Mmanga amemuahidi Waziri Prof. Mbarawa kufanya kazi kwa uadilifu, bidii, na kuzingatia thamani ya fedha katika miradi yote inayotekelezwa na wakala.
 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni