Jumatano, 5 Aprili 2017

SERIKALI YASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO WA ANGA.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Sam Kutesa (kushoto), wakisaini mkataba wa ushirikiano katika masuala ya anga baina ya nchi hizo mbili, jijini Arusha.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), akibadilishana hati za makubaliano na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Sam Kutesa (kushoto), kuhusu ushirikiano katika masuala ya anga baina ya nchi hizo mbili, jijini Arusha.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda, Sam Kutesa (kushoto), wakionesha hati zao za makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya anga baina ya nchi hizo, jijini Arusha. Mkataba huo utaimarisha huduma za usafiri na usalama wa anga.
 
Serikali ya Tanzania na Uganda zimesaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano (BASA), katika usafiri wa anga utakaowezesha nchi hizo kutoa huduma bora za anga  na kufungua fursa za kibiashara kwa wananchi wake.

Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo jijini Arusha, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema mkataba huo utaruhusu ndege za nchi hizo mbili kutua na kuruka bila vikwazo vyovyote katika nchi hizo.

"Naamini ushirikiano huu utaboresha huduma zinazotolewa na Mamlaka za usafiri wa Anga na hivyo kuongeza viwango vya  usalama wa usafiri huu", amasesema Prof. Mbarawa.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda,  Sam Kutesa, amesisitiza kuwa mkataba huo ni muendelezo wa ushirikiano mwema baina ya Tanzania na Uganda na hivyo kuchochea maendeleo ya uchumi kwa raia wa nchi hizo.

Ushirikiano wa Tanzania na Uganda ni sehemu ya mkakati wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuwezesha wananchi wake kunufaika na fursa za kijamii, kiuchumi, kiusalama na kiutamaduni.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni