Jumatano, 19 Aprili 2017

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA RELI YA KISASA STANDARD GAUGE KUTOKA DAR HADI MOROGORO

Mfano wa Reli ya Kisasa ya Standard Gauge SGR itakayojengwa kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro na baadae kuendelea hadi mikoa ya Mwanza na Kigoma.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akitoa hotuba ya utangulizi wakati wa Uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Reli ya Kisasa, (SGR), uliofanyika Pugu nje kidogo ya Mji wa Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho, akiwatambulisha wageni waliohudhuria kwenye halfa ya  Uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Reli ya Kisasa, (SGR), uliofanyika Pugu nje  kidogo ya Mji wa Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Jospeh Magufuli (watano kulia waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi walio chini ya WIzara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, mara baada ya Uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Reli ya Kisasa, (SGR), uliofanyika Pugu nje kidogo ya Mji wa Dar es Salaam. Kulia kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Jospeh Magufuli akifunga  karatasi maalum kuashiria Uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi waReli ya Kisasa, (SGR) kuanzia Dar es Salaam Mpaka Morogoro kilomita 300, uliofanyika Pugu nje kidogo ya Mji wa Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Jospeh Magufuli (mwenye suti ya bluu) akifurahi jambo na Waziri waUjenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, ProfesaMakame Mbarawa (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Miliki ya Rasilimali za Reli (RAHCO) Bw. Masanja Kabogosa (kulia) katika hafla ya Uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Reli ya Kisasa, (SGR) kuanzia Dar es Salaam Mpaka Morogoro kilomita 300, uliofanyika Pugu nje ya Kidogo ya Mji wa Dar es Salaam.

Wajumbe wa Kamati maalum ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), wakitambulishwa kwa Mgeni Rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Jospeh Magufuli (hayupo pichani) wakati wa Uwekaji wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa Reli hiyo uliofanyika Pugu nje ya kidogo ya Mji wa Dar es Salaam.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni